Na VENANCE JOHN
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump hapo jana amesema mara atakapokuwa rais atachukua hatua ya kuwaweka wanaume mbali na michezo ya wanawake hasa wale waliobadili jinsi kutoka wanaume kuwa wanawake. Trump ameahidi wakati wa kampeni yake ya kuzuia huduma ya kuthibitisha jinsia na ushiriki wa michezo ya watu waliobadili jinsi.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_446acc2ca46d49ebbb483bae96931156~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_446acc2ca46d49ebbb483bae96931156~mv2.jpeg)
Pia Trump amesema kwamba atatoa hati za siri katika siku zijazo zinazohusiana na mauaji ya Rais wa zamani wa Marekani, John F. Kennedy, Seneta Robert Kennedy na kiongozi wa haki za kiraia Martin Luther King Jr.
Trump, ambaye anarejea Ikulu ya White House leo kwa kuapishwa, ameahidi kutoa faili za siri za kijasusi na utekelezaji wa sheria kuhusu mauaji ya John F. Kennedy ya 1963, akiwa rais wa 35 wa Marekani.
"Katika siku zijazo, tutaweka hadharani rekodi zilizosalia zinazohusiana na mauaji ya Rais John F. Kennedy, kaka yake Robert Kennedy, na Dk. Martin Luther King Jr. na mada zingine zenye maslahi makubwa kwa umma," Trump hakubainisha ni nyaraka zipi zitatolewa, na hakuahidi kufutiliwa mbali. Martin Luther King Jr. na Robert Kennedy wote waliuawa mwaka 1968.
Kennedy Jr, ambaye ni mtoto wa Robert Kennedy na mpwa wa John F. Kennedy, amesema anaamini shirika la upelelezi (CIA) lilihusika katika kifo cha mjomba wake, madai ambayo shirika hilo limeeleza kuwa hayana msingi.
Opmerkingen