top of page

TRY AGAIN AMUOMBA MO AWE MWENYEKITI WA BODI

Taarifa kwa Umma iliyotolewa na klabu ya Simba SC inaeleza kuwa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene maarufu Try Again ametangaza kujiuzulu wadhifa huo hii leo.

Try Again ametangaza maamuzi hayo yenye lengo la kutoa nafasi kwa klabu ya Simba kuwa na



mwanzo mpya ulio bora zaidi.

Katika hatua nyingine Try Again amemuomba Mwekezaji na Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed Dewji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.

Baada ya kutangaza uamuzi huo Try Again, amewaomba Wanachama, Mashab- iki na Wapenzi wa Simba kuvunja makundi yote na kuwapa ushirikiano viongozi kwa maslahi ya klabu yetu.

Salim Abdallah Muhene amehudumu katika Bodi ya Wakurugenzi ya Simba kwa kipindi cha miaka saba akiwa Mjumbe, Makamu Mwenyekiti na baadae Mwenye- kiti wa Bodi hiyo

Akihitimisha taarifa ya kujiuzulu kwake, Try Again amemshukuru Rais wa Heshi- ma Mohammed Dewji kwa kumpa nafasi ya kuongoza klabu hii, Wana Simba wote, Taasisi za mpira na Serikali.



Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page