Kutoka kwenye ukurasa wa Haji Manara ameandika ujumbe huu
"Toka lini Wakuu wa Mikoa wanazuiwa kuzisapoti Team za mikoa wanayoiongoza?
RC Mtanda ni kiongozi wa kwanza kuipa sapoti Team ya mkoa wake?, Na Why ihusishwe Yanga?, Je, Mh. @said_mtanda kuwa mshabiki wa Wananchi ni dhambi? . Mbona tushaona Ma RC wengi wakijinadi na Makolo na wanaisapoti?
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_3c637e7b9bff47eba14a8ee92f2453b4~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_3c637e7b9bff47eba14a8ee92f2453b4~mv2.jpeg)
Mkuu wa Mkoa ndie Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa husika, akienda mahali na vyombo vyake vya usalama ni kuhujumu team pinzani?
Likitokea lakutokea nani ataulizwa?
Tucheze Mpira bhana, tusitafute huruma na Visingizio, Team ya kuifunga @pambajijifootballclub mnayo hata RC asipotaka. Ukubwa wenu upo wapi sasa kama mnadeka deka hadi kwa Wasukuma? Nyie c mlisema huu mwaka wa Ubaya Ubwege @said_mtanda kanyaga twende usicheke na wowote".
Comments