Na VENANCE JOHN
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_9a699d18f2204753a6d6e698af5c4e2f~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_9a699d18f2204753a6d6e698af5c4e2f~mv2.jpeg)
Waziri wa nishati nchini Sri Lanka, Kumara Jayakody amelaumu tumbili kwa kusababisha kukatika kwa umeme kote nchini humo kwa madai kuwa aliingia kwenye kituo cha uzalishaji umeme kusini mwa mji mkuu wa Colombo.
Umeme umeshaanza kurejeshwa taratibu katika taifa hilo lenye watu milioni 22, huku vituo hosipitali na mitambo ya kusafisha maji vikipewa kipaumbele. "Tumbili aligusa transfoma ya gridi yetu, na kusababisha kukosekana kwa usawa katika mfumo wa umeme," Waziri wa Nishati Kumara Jayakody amewaambia waandishi habari.
Comments