Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amechapisha taarifa isemayo
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_c9f0a3fafb644ff798744c7538ef2628~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_c9f0a3fafb644ff798744c7538ef2628~mv2.jpeg)
"Baada ya kazi nzuri kwa kipindi cha mwaka mzima, leo Disemba 20, 2024 tumekabidhi rasmi nyumba 109 kwa ndugu zetu walioathiriwa na maporomoko ya tope mwezi Disemba mwaka jana wilayani Hanang, mkoani Manyara.
Uamuzi wa kujenga nyumba hizi umelenga kuwasaidia ndugu zetu hawa kurejea katika hali yao ya kawaida ya maisha baada ya changamoto ile, ambapo baadhi walipoteza ndugu, jamaa na marafiki, na wengine kupoteza kila walichokuwa nacho.
Nawatakia kila la kheri."
Comments