top of page

TUTAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI - RAIS SAMIA

Ikiwa leo ni siku ya Wafanyakazi Mei Mosi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha ujumbe huu

"Kheri ya Siku ya Wafanyakazi kwenu nyote. Siku hii ni ya mambo makubwa mawili. Jambo la kwanza ni kwa sote kuwashukuru wale ambao kwa kazi zao sisi kama Taifa tunaweza kusonga



mbele; kuanzia dada wa kazi hapo nyumbani anayeamka mapema alfajiri kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, hadi daktari anayehakikisha tunapata tiba pale tunapokuwa na changamoto ya maradhi. Tunawashukuru nyote katika kila kona ya nchi yetu. Ahsanteni kwa kazi."

Jambo la pili, leo pia ni siku ya kurudia ahadi yetu kwenu. Ahadi ambayo kila wakati tumekuwa tukiitoa na kuitekeleza kadiri tuwezavyo. Ahadi kwamba kama Serikali tutaendelea kutekeleza jukumu letu la msingi kuhakikisha mazingira ya kazi yanazidi kuwa bora zaidi kwa kila mmoja si tu mishahara, bali pia haki katika maeneo ya kazi, kupanda madaraja kwa wakati, kupata stahiki sahihi na uboreshaji wa mifumo yetu ya pensheni.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page