Na VENANCE JOHN
Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv nchini Ukraine umepokea taarifa kuhusu uwezekano wa kutokea shambulizi kubwa la anga siku ya leo na utafungwa. Taarifa hii ni kutoka Idara ya Masuala ya Ubalozi wa Marekani.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_f52fda3e24314dd9949f70b548198614~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_f52fda3e24314dd9949f70b548198614~mv2.jpeg)
"Kutokana na wingi wa tahadhari, ubalozi utafungwa, na wafanyakazi wa ubalozi wanaagizwa kujikinga," idara hiyo ilisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya ubalozi wa Marekani mjini Kyiv. "Ubalozi wa Marekani unapendekeza raia wa Marekani kuwa tayari kujihifadhi mara moja katika tukio ambalo tahadhari itatangazwa." Ilisisitiza taarifa hiyo.
Onyo hilo linakuja siku moja baada ya Ukraine kutumia makombora ya ATACMS ya Marekani kushambulia eneo la Urusi, ikitumia fursa ya ruhusa mpya iliyotolewa na utawala unaoondoka wa Rais wa Marekani Joe Biden katika siku ya 1,000 ya vita.
Urusi ilikuwa ikizionya nchi za Magharibi kwa miezi kadhaa kwamba iwapo Washington itairuhusu Ukraine kurusha makombora ya Marekani, Uingereza na Ufaransa hadi ndani kabisa ya Urusi, Moscow ingewachukulia wanachama hao wa NATO kuhusika moja kwa moja katika vita vya Ukraine.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema mwezi Oktoba kwamba Moscow itajibu mashambulizi Siku ya jana Jumanne, Putin alisaini amri mpya ambayo inamruhusu kushambulia ka kutumia nyuklia kujibu mashambulio ya kawaida, huku hatari za nyuklia zikiongezeka huku kukiwa na mvutano mkubwa kati ya Urusi na Magharibi katika zaidi ya nusu karne kuhusu vita vya nyuklia.
Comentários