top of page

UFARANSA YATOA WARANTI KWA MARA YA PILI WA KUKAMATWA KWA BASHAR AL-ASSAD ALIYEKUWA RAIS WA SYRIA

Na VENANCE JOHN


Mahakimu wawili nchini Ufaransa wametoa waranti wa kukamatwa kwa rais aliyeondolewa madarakani wa Syria, Bashar al-Assad kwa madai ya kuhusika katika uhalifu wa kivita. Hii ni hatua ya pili kuwahi kuchukuliwa na mamlaka za haki za Ufaransa.


Waranti huo wa kukamatwa umetolewa kama sehemu ya uchunguzi wa mauaji ya mwalimu wa zamani raia wa Ufaransa aliyekuwa na uraia wa Syria na Ufaransa. Salah Abou Nabout aliyekuwa na umri wa miaka 59, aliuwawa 7 tarehe June mwaka 2017 kufuatia kulipuliwa kwa nyumba yake na helikopta za jeshi la Syria


Kulingana na chanzo kimoja, ídara ya mahakama ya Ufaransa inachukulia kwamba Assad ndiye aliyeamrisha na kufadhili kufanyika kwa shambulizi hilo. Maafisa wengine sita waandamizi katika jeshi la Syria tayari wametolewa waranti wa kukamatwa kuhusiana na kesi hiyo katika uchunguzi ulioanza mwaka 2018.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page