NA VENANCE JOHN
Uganda imethibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa virusi vya Ebola katika mji mkuu Kampala, huku mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa akiwa tayari amefariki kutokana na ugonjwa huo Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya afya hii leo ambapo imesema mgonjwa huyo alifarikia hapo jana.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_6912fd17d0e54d0d918659efd464d434~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_6912fd17d0e54d0d918659efd464d434~mv2.jpeg)
Mgonjwa huyo, ambaye alikuwa ni muuguzi katika hospitali ya rufaa ya Mulago katika mji mkuu, awali alikuwa ametafuta matibabu katika vituo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mulago baada ya kupata dalili kama za homa.
“Mgonjwa alipata shida ya kushindwa kufanya kazi kwa viungo vingi na alifariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa ya Mulago mnamo Januari 29. Sampuli za uchunguzi wa maiti zilithibitisha Ugonjwa wa Virusi vya Ebola vya Sudan” wizara ilisema katika taarifa yake.
Homa hiyo inayoambukizwa kwa haraka sana ambayo dalili mojawapo ni kuvuja damu huambukizwa kwa kugusana na majimaji ya mwili na tishu zilizoambukizwa. Dalili nyinginezo ni pamoja na maumivu ya kichwa, kutapika damu, maumivu ya misuli.
Uganda ilikumbwa na mlipuko mara ya mwisho mwishoni mwa 2022 na mlipuko huo ulitangazwa kuisha Januari 11, 2023 baada ya takriban miezi minne ambapo ilijitahidi kudhibiti maambukizi ya virusi. Mlipuko wa mwisho uliua watu 55 kati ya 143 walioambukizwa na waliokufa ni pamoja na wafanyakazi sita wa afya.
Comments