Na VENANCE JOHN
Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer amesema yuko radhi na tayari kupeleka wanajeshi wa Uingereza nchini Ukraine kusaidia kuhakikisha usalama kama sehemu ya makubaliano ya amani.

Sir Keir amesema amani ya kudumu nchini Ukraine ni muhimu ikiwa wanataka kumzuia Rais Putin asiendelee na uchokozi zaidi siku zijazo. Kabla ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa viongozi wa Ulaya mjini Paris leo Jumatatu, Sir Keir amesema Uingereza iko tayari kuchangia katika dhamana ya usalama wa Ukraine kwa kupeleka wanajeshi wake Ukraine ikiwa itahitajika.
Sir Keir amesema wanajeshi wa Uingereza wanaweza kupelekwa kandokando ya mpaka kati ya maeneo yanayoshikiliwa na Ukraine na yale yanayoshikiliwa na Urusi, wakiungana na wanajeshi kutoka mataifa mengine ya Ulaya.
Comments