Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za masoko duniani ikiwemo ya jarida la "Wealth", simu kutoka kwenye kampuni ya Apple yaani IPhone, kwa sasa zinakabiliwa na upungufu wa 23% kwenye uingizwaji wake kuelekea bara la Asia, hasa nchini China, ambapo ushindani mkali kutoka kwa chapa kama Xiaomi, Samsung, na Huawei ukizidi kubadilisha soko.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_440d429ba8f84b47bf52b754c3734b9c~mv2.jpg/v1/fill/w_526,h_526,al_c,q_80,enc_avif,quality_auto/57c8da_440d429ba8f84b47bf52b754c3734b9c~mv2.jpg)
Katika robo ya pili ya mwaka wa 2024, Apple ilitolewa kwenye orodha ya wauzaji wakuu wa simu nchini China, huku Samsung na Xiaomi wakitumia fursa hiyo na kuonesha ukuaji katika masoko muhimu.
Changamoto ya Apple inaweza kutolewa kwa sehemu na mabadiliko ya vipaumbele vya watumiaji wa simu zinazoweza kuwa na vitu pendwa zaidi ambavyo vinavyotolewa na washindani, na kusukuma chapa kama Samsung na Xiaomi kuwa kwenye nafasi zenye nguvu zaidi.
Comments