Ujenzi wa mnara wa Jeddah wenye urefu wa kilometa moja nchini Saudi Arabia, ambao utakuwa jengo refu zaidi duniani ukikamilika, umeanza tena takribani miaka saba baada ya kusitishwa.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_16f30d69985f47c7a757d6f80ebe7131~mv2.jpg/v1/fill/w_526,h_526,al_c,q_80,enc_avif,quality_auto/57c8da_16f30d69985f47c7a757d6f80ebe7131~mv2.jpg)
Mnara huo ulibuniwa na mbunifu wa Marekani Adrian Smith, ambaye alitumia alama ya sehemu ya ua ya petali (petal) na umbo jembamba chini na pana juu (aerodynamic shape) ili kukabiliana na changamoto kubwa za kiufundi za kujenga katika urefu kama huo.
Katika hafla iliyofanyika kwenye eneo linapojengwa jingo hilo, hapo jana muungano wa makampuni yaliyo nyuma ya mradi huo, Jeddah Economic Company (JEC), ulitangaza kuwa mnara huo sasa umepangwa kukamilika mwaka 2028.
Jumba hilo ambalo hapo awali liliitwa Kingdom Tower, lilibomoka mwaka wa 2013 na lilitarajiwa lingekamilika mwaka 2020. Ikiwa ujenzi wake utakamilka litakuwa zaidi ya futi 500 kuzidi jengo la Burj Khalifa la Dubai, ambalo kwa sasa ndilo jengo refu zaidi duniani.
Jumba hilo lina urefu wa mita 1,000 (km 1)kuelekea juu na lilisimama ujenzi wake mwaka 2017, baada ya watu kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na wenyeviti wa makampuni yenye kandarasi kuu na mfadhili mwenza wa mradi huo walipokamatwa na mwana mfalme Mohammed Bin Salman
Hatua hiyo ilikuja kufuatia kampeni ya Bin Salman ya kupinga ufisadi, ambayo ilishuhudia mamia ya watu wakihojiwa juu ya tuhuma za ufisadi.
Sherehe za wiki hii zilihudhuriwa na mmoja wa maafisa waliowekwa kizuizini hapo awali, Mwanamfalme wa Saudia, Alwaleed bin Talal, ambaye ni mwenyekiti wa Kampuni ya Kingdom Holding, mmoja wa waungaji mkono wakuu wa mradi huo.
Alwaleed, binamu wa mwana mfalme, aliachiwa karibu miezi mitatu baada ya kukamatwa kwake, ingawa haijulikani kwa nini na chini ya hali gani aliachiwa. Kufuatia sherehe ya jana, Alwaleed alichapisha video kwa X inayoonyesha toleo la mnara huo unaomeremeta na kuandika "Tumerudi."
Comments