
Prophet Kabozyangilia, moja ya vijana wapambanaji wanaozidi kuonesha uzalendo wao kwa taifa la Tanzania, ametoa ujumbe huu mzito kwa vijana wote nchini.
NUKUU, "kwa majina naitwa Prophet Kabozyangilia, kiongozi wa umoja wa vijana wa Malkia wa Tanzania na pia Mbunifu wa Nembo ya Malkia wa Tanzania. Vijana wenzangu poleni na majukumu ya kulijenga taifa letu mimi kama kijana mwenzenu naombeni tushirikiane kwa pamoja kumuunga mkono Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, mama huyu ametufanyia mambo makubwa sana yenye kuleta maendeleo kwenye taifa hili na maendeleo hayo yanaonekana nitayataja baadhi kwa kuwa ni mengi sana:-
1- Aliweza kujenga madarasa mapya ya shule zote nchini tena kwa muda mfupi.
2 - Ametoa mikopo kwa vijana, walemavu, kina mama na watu wa rika zote lengo lake kila mwananchi ajikwamue kiuchumi pia rais wetu hapendi kuona mwananchi wake akiishi bila matumaini ndio maana anapambana huku na kule ili tu watanzania wapate huduma zote muhimu
3- Ameleta wawekezaji sehemu nyingi takribani nchi nzima hiyo imesaidia vijana kutapata ajira kwa wingi lakini hata mnaofanya biashara mtapata bidhaa hapa hapa badala kutoa nje ya nchi,tumpongeze mama,pia vijana tuache kufuata mkumbo wa kulalamika unaoletwa na watu wachache wenye lengo tofauti kwa maslahi yao.
Hivyo sasa kwa unyenyekevu mkubwa naomba tuungane kumsapoti Rais ili atufanyie maendeleo makubwa zaidi lakini pia ifikapo 2025 tuondoke na Rais wetu kuelekea awamu nyingine ya 2026 hadi 2030 pia tukimaliza uchanguzi mimi kama kijana mwenzenu nitaongoza vijana wote nchi nzima kuomuomba mama atuongezee mikopo iwe zaidi ya sasa ili vijana wengi iwafikie mpaka vijijini, hivyo badala ya mikopo ya mateso makubwa ya mitaani inayorudisha nyuma maendeleo ya watanzania wengi kwa masharti magumu, sasa Rais atatukopesha mikopo ya bila masharti magumu. Ndugu zangu baada kusema hayo naomba sana ushirikiano mkubwa kwa Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan, MUNGU awabarki sana na ambariki Rais wetu na amuongezee umri na kuimarisha afya yake Ameen".
Comments