top of page

UKIAMBIWA KUNA CHOKOLETI INATENGENEZWA KWA MABAKI YA CHAKULA KILICHOTUPWA UTAENDELEA KULA?

Na VENANCE JOHN


Unaweza kufikiri kuna utani, lakini huu si utani hata kidogo kwamba baadhi ya vyakula tunavyokula vinatonakana na makombo (mabaki) ambayo yangetakiwa kutupwa. Maeneo mengi ya Ulaya, Amerika na Asia, bidhaa za chakula kilichotumika, na hata kutupwa sasa zinapewa maisha ya pili na kuliwa upya.





Katika jengo la ghorofa mbili katika bandari ya Refshaleøen, mjini Copenhagen, kuna kijana kwa jina Rasmus Munk ni mpishi mwenye dhamira ya kusafisha chakula kichotupwa kuwa tena chakula. Rasmus Munk ni mmoja ya watu wengi wanaoamini kwamba nyakati zijazo, chakula kitategemea kile ambacho tayari tumekitupa.


Katika maabara ya Spora, maabara ambayo iko mita chache kutoka mkahawa wa Rasmus Munk, kunatengezwa chokoleti iliyopewa jina la Alchemist, chokoleti inayotokana na maganda ya kakao.


Maabara hii ilitokana na majaribio yaliyofanywa na kampuni ya Alchemist, ambayo inalenga hasa matumizi ya bidhaa za wanyama zinazopuuzwa kama vile samaki aina ya jellyfish au vichwa vya kuku vilivyokaangwa sana hivyo kuharibika.


Bidhaa za vyakula vilivyokwisha tumika kwa sasa zinatengeneza mkate, tambi na virutubisho vingine kutoka katika nafaka zilizotumiwa ambazo kawaida hutupwa baada ya kuzalisha bia na kahawa lakini kwa sasa zinachakatwa tena upya na kuwa pombe kali, unga na hata vyakula kama chokololeti. Bidhaa zingine zinazotengenezwa kwa sasa ni pamoja na biskuti, na unga wa kuoka baadhi ya vitafunwa.


Tafiti zinaonesha kuwa karibu 8% ya uzalishaji wa gesi chafu duniani unasababishwa na chakula kilichotupwa au kuharibika na karibu 40% ya vyakula vyote vinavyokuzwa Marekani kila mwaka hutupwa. Kwa hivyo ili kukabiliana na tatizo hilo watu wameanza kubuni namna ya kusaidia kuunda chakula kipya kutoka kwenye mabaki yaliyokwisha tupwa.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page