Wanajeshi wa Korea Kaskazini wamepambana na wanajeshi wa Ukraine kwa mara ya kwanza baada ya takribani wanajeshi 11,000 wa Kikorea kuingia Ukraine

Hayo yamejiri baada ya maafisa wakuu wa Ukraine kufichua taarifa hiyo katika mahojiano na shirika la utangazaji la Korea Kusini KBS. Aidha Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov amesema kuwa kundi dogo la wanajeshi wa Korea Kaskazini limeshambuliwa
Kwa upande wake Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa mpaka sasa Nchi za Magharibi hazijajibu chochote kuhusu kuingia kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini na vita hivyo kufungua sura mpya ya ukosefu wa utulivu duniani.
Comments