Na VENANCE JOHN
Ukraine leo inaadhimisha siku 1,000 tangu uvamizi kamili wa Urusi, huku wanajeshi waliochoka wakipambana katika nyanja nyingi, Ukraine ikizingirwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya ndege zisizo na rubani na makombora. Huku pia wasiwasi ukizidi kupanda kwa Donald Trump kurejea ikulu ya White House mwezi Januari kwani alishaonesha kuwa hatokuwa tayari kuendelea kutoa misaada kwa Ukraine.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_4fd9cfe61d504262a8e9a2d4f0ee19e9~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_4fd9cfe61d504262a8e9a2d4f0ee19e9~mv2.jpeg)
Katika kuimarisha nchi hiyo iliyokabiliwa na mzozo, Rais wa Marekani Joe Biden alitoa ruhusa kwa makombora ya Marekani kutumika dhidi ya shabaha zilizo ndani zaidi ya Urusi, na hivyo kutimiza ombi la muda mrefu la Ukraine.
Lakini mabadiliko makubwa ya sera yanaweza kubadilishwa wakati Trump atakaporejea Ikulu ya White House mwezi Januari, na wataalam wa kijeshi wanaonya kwamba hiyo inaweza kubadilisha mkondo wa vita vya ambayo vimedumu kwa miezi 33.
Maelfu ya raia wa Ukraine wamekufa, zaidi ya milioni 6 wanaishi kama wakimbizi nje ya nchi na idadi ya watu imepungua kwa robo tangu kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin kuamuru uvamizi wa nchi kavu, baharini na angani.
Hata hivyo ni kama Ukraine imeanza kunyoosha mikono kukubali yaishe kwani Rais Volodymyr Zelenskiy alisema wiki iliyopita kwamba Ukraine lazima ifanye kila iwezalo kumaliza vita mwaka ujao kwa njia za kidiplomasia.
Lakini kwa puande wake Urusi inasema malengo yake ya vita bado hayajabadilika kwani mwezi Juni rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kwamba Ukraine lazima iondoe matamanio yake ya kujiunga na NATO, na lazima Ukraine ijiondoe katika maeneo yake 4 ambayo majeshi ya Urusi yanadhibiti kwa kiasi, hii ikiwa ni ni sawa na kusalimu amri kwa Ukrane.
Comments