top of page

UKRAINE YASEMA IMEWAUA WANAJESHI WA KOREA KASKAZINI KATIKA MAPIGANO MKOA WA KURSK

Na VENANCE JOHN


Idara ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine na ile ya Marekani, Pentagon zimesema kuwa wanajeshi wa Ukraine wamewaua na kuwajeruhi idadi kadhaa ya wanajeshi wa Korea Kaskazini wanaopigana pamoja na vikosi vya Urusi katika eneo la mpaka wa Kursk.


Shirika la kijasusi la kijeshi la Ukraine, linalojulikana kama GUR, limesema kwamba vikosi vya jeshi la Korea Kaskazini vimepata hasara kubwa na askari 30 waliuawa na kujeruhiwa katika eneo la Kursk, karibu na vijiji vya Plekhovo, Vorobzha na Martynovka na kwamba katika eneo la kijiji cha Kurilovka, angalau wanajeshi watatu wa Korea Kaskazini walitoweka.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Washington, DC, msemaji wa Pentagon Meja-Jenerali Pat Ryder aliunga mkono madai ya Jeshi la Ukraine, akisema kwamba Marekani imepata dalili kwamba wanajeshi wa Korea Kaskazini wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano huko Kursk.


Ikulu ya Urusi Kremlin, ambayo mara chache hutoa maelezo juu ya majeruhi kati ya askari wake na wale wa washirika wake haikuwa tayari kusema chochote juu ya madai hayo baada ya kuombwa na shirika la habari la habari la Associated Press


Kwa mujibu wa taarifa za kijasusi za Korea Kusini, Marekani na Ukraine, takriban wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wametumwa Urusi kupigana kwenye mstari wa mbele dhidi ya vikosi vya Ukraine.

留言


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page