Na VENANCE JOHN
Ukraine imeanza kutumia mifumo kadhaa iliyoboreshwa ya akili mnemba (Artificial Intelligence; AI) mifumo itakayowekwa ndani ya ndege zake zisizo na rubani ili kufikia shabaha kwenye uwanja wa vita dhidi ya Urusi
Mifumo ya sasa inayotumia akili mnemba huiruhusu ndege zisizo na rubani za bei nafuu zinazobeba vilipuzi kubaini au kuruka kwenye maeneo yanayolengwa katika maeneo yanayokuwa na msongamano mkubwa wa mawimbi, jambo ambalo limepunguza ufanisi wa ndege zisizo na rubani zinazoendeshwa kwa mikono.
Mabadiliko kuelekea utumiaji wa akili mnemba haswa katika kutafuta shabaha na udhibiti wa droni, ni hatua muhimu inayoibuka katika mbio za teknolojia ambazo zimejitokeza tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake kamili dhidi ya jirani yake Ukraine mwezi Februari 2022.
Mfumo huo unalenga kutumia droni kushambulia adui bila kuendeshwa na binadamu kama ilivyo droni nyingi ambazo huhitaji mtu kuwa na kifaa maalum kinamwezesha kuiongoza droni na kufikia shambaha inayolengwa.
Commentaires