top of page

UKWELI KUHUSU SAKATA LA CLEMENT MZIZE - JEMEDARI SAID

Kutoka kwa Mchambuzi wa michezo Jemedari Said amefunguka haya juu ya sakata la Mchezaji wa Yanga SC Clement Mzize kuhusishwa na Azam FC

"Jumatatu tarehe 15 April 2024 uongozi wa Azam FC @azamfcofficial ulipeleka ofa kwa klabu ya Yanga SC @yangasc wakitaka kumsajili mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Clement Mzize, ofa ya Azam FC ni Ths 400,000,000/= (400M), baada ya kupokea ofa hiyo siku iliyofuata yani Jumanne tarehe 16 April 2024, uongozi wa Yanga ukaijibu barau ya Azam FC kwamba wao


kama viongozi watakaa na kujadili ofa hiyo kisha watawajibu.

Kwenye ofa ya Azam FC hakuna sehemu yoyote ambayo imezungumzia suala la kubadilishana wachezaji (swap deal) kati ya Clement Mzize na Prince Dube ambaye yupo kwenye matatizo na Azam FC. Azam FC wamepokea maelekezo ya kocha wao kwamba anataka washabuliaji 2 mmoja mzawa na mwingine mgeni, mzawa anamtaka Mzize. Ndipo vongozi wa Azam FC wakatoka na ofa ya 400M, HAKUNA KUBADILISHANA WACHEZAJI.

Kilichotokea baada ya Azam FC kuweka pesa mezani, Mzize kaingiziwa pesa za kuongeza mkataba na klabu yake ya Yanga ambapo bado wapo kwenye maongezi ya mkataba mpya.

Watu wa karibu yake wamethinitisha hili na habari zinasema huenda muda wowote Clement Mzize ataongeza mkataba na Mabingwa wa nchi. Kama ana wasimamizi imara manake ni kwamba anaweza kuzoa zaidi ya 400M kutoka Yanga, Kwani Azam wako mlangoni. Ila kwa kariba ya wachezaji wetu utakuja kusikia kituko utaziba uso.

NB: Mzize anahusishwa na kutakiwa na klabu ya Watford ya

England, lakini Mzize pia aliwahi kuhusishwa kutakiwa na

klabu ya Marseille ya Ufaransa, akili kichwani mwake na

wanaomzunguka." Ameandika Jemedari.


댓글


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page