top of page

UMEUMIZA MIOYO YA WANASIMBA LAKINI WEWE SIO WA KWANZA - AHMED ALLY

Huu ndio ujumbe wa Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally kwenda kwa mchezaji Chasambi.


"Rasmi leo ndio umekua mtu mzima wa kimpira, ingekua kimaumbile tungesema umebaleghe hii leo. Matusi, kejeli, na dhihaka zote utakazopokea leo ni ukaribisho kwenye ukubwa wako, yasikutishe tamaa na wala yasikuvunje moyo, KARIBU UKUBWANI


Umeumiza mioyoo ya Wana Simba, lakini wewe sio wa kwanza kwenye mpira, wapo wenzio makosa yao yaliwanyima Kombe la Dunia. Kosa hili linakuongezea ukomavu. Ndugu zangu Wana Simba najua tunahisira na kijana wetu lakini kila mtu kazini kwake anakosea


Na tukumbuke kabla ya kujifunga alishaisaidia timu kupata goli hivyo sukari na chumvi vimechanganyikana hii leo na bahati mbaya chumvi imezidi. Tukasirike lakini tusimchukie, na kama haitoshi tumsamehe na tuanze kumtia moyo


Kipindi hiki anatuhitaji zaidi sisi familia yake kumtetea na kumpigania ili arejee kwenye utulivu wake wa kiakali na aendelee kuipigania Simba yetu. Tunapatia pamoja, tunakosea pamoja, tunajisahihisha pamoja tunasonga mbele" Ahmed Ally.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page