Na VENANCE JOHN
Nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika zitakutana kesho Ijumaa mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia, kwa ajili ya kumchagua mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja huo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_f079f0b631174d7598ca1da3dcad8a13~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_f079f0b631174d7598ca1da3dcad8a13~mv2.jpeg)
Kabla ya mkutano mkuu, viongozi hao watafanya kikao cha dharura kujadili machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo waasi wa M23 wanakalia maeneo muhimu baada ya kushinda majeshi ya serikali.
Katika mkutano huo mkuu moja ajenda kuu ni kufanya uchaguzi wa kumsaka mwenyekiti wa kamisheni Umoja wa Afrika ambapo mwanasiasa mkongwe kutoka Kenya, Raila Omolo Odinga naye yuko kwenye kinyang’anyiro akichuana na waziri wa mambo ya nje wa Djibouti, Mahmoud Ali Youssouf na Richard Randriamandrato kutoka Madagascar. Msindi atapatikana kupitia kupiga kura ya siri
Katika wadhifa huo, mshahara ni dola 15,576 kila mwezi, huku watoto wa mtu anayeshikilia wadhifa huo wakigharamikiwa elimu yao kikamilifu na Umoja wa Afrika. Uchaguzi huo unakuja baada ya mwenyekiti anayeondoka ofisini Moussa Faki Mahamat kukamilisha mihula yake miwili. Faki amehudumu tangu 2017.
Comments