top of page

UMOJA WA MATAIFA WATOA SIKU 21 ISRAEL KUMALIZA VITA, ITAWEZEKANA?

Rais wa Marekani Joe Biden amesema haamini kama kutakuwa na "vita vya hali ya juu tena" Mashariki ya Kati, licha ya Israel kulipiza kisasi baada ya shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa Tehran.


Biden amesema mikakati mingi zaidi inahitajika kufanywa ili kuepusha vita vinavyozidi kutokea Mashariki ya Kati, wakati ambapo jeshi la Israel linaipiga Beirut kwa mashambulizi mapya ya anga katika vita vyake dhidi ya kundi la Lebanon la Hezbollah.


Alipoulizwa na waandishi wa habari mjini Washington jinsi alivyo na uhakika kwamba vita vinaweza kuepukika, Biden amesema, " Nadhani tunaweza kuiepuka, lakini kuna mambo mengi bado ya kufanya, nasisitiza mambo mengi ya kufanya bado."


Wakati Marekani, Umoja wa Ulaya na washirika wengine wakitoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano kwa siku 21 katika mzozo wa Israel na Lebanon, Biden amesema Marekani inajadiliana na Israel kuhusu chaguzi zake za kujibu mashambulizi ya Tehran, ambayo ni pamoja na Israel kushambulia vifaa vya mafuta vya Iran. Alinukuliwa Biden akizungumza na waandishi wa habari.


Kauli na maoni ya rais Biden, yamechagiza ongezeko la bei ya mafuta duniani, pamoja na kuongezeka kwa mvutano wa mataifa ya Mashariki ya Kati kumewafanya wafanyabiashara kuwa na wasiwasi kuhusu kukatika kwa usambazaji wa bidhaa.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page