Msemaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani, nchini DRC, Shelley Thakral, amesema hatua hii ni ya muda hata hivyo akielezea wasi wasi kuhusu raia kuendelea kukosa chakula ikiwa mapigano yataendelea kwa muda mrefu.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_947496bf1c3b496cb0d22942612196fe~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_947496bf1c3b496cb0d22942612196fe~mv2.jpeg)
Amesema hali hii ni kipimo kwa watu ambao wamefungiwa kutokana na mapigano hayo akisema saa 24 zitakazofuata zitakuwa za changamoto kubwa watu wakilazimika kuona namna ya kujikimu.
Aidha umoja wa Mataifa unasema hospitali kwenye mji wa Goma zimeendelea kuzidiwa uwezo kutokana na idadi kubwa ya majeruhi waliopigwa risasi pamoja na kutapakaa kwa miili ya watu waliouawa kwenye mitaa ya jiji hilo. Katika hatua nyingine, shirika linalohudumia wakimbizi limeonya kuwa huenda mzozo huu ukaenea kwenye ukanda.
Comentarios