top of page

UPINZANI NCHINI VENEZUELA WADAI KUSHINDA UCHAGUZI HUKU BARAZA LA UCHAGUZI LIKIMTANGAZA RAIS NICOLAS MADURO KUWA MSHINDI

Na VENANCE JOHN


Upinzani nchini Venezuela wanadai kuwa wameshinda uchaguzi wa urais nchini humo na kutengeneza msigano na serikali ambayo mamlaka zinazosimamia uchaguzi zimemtangaza rais Nicolás Maduro ambaye alikuwa anatetea kuingia Ikulu kwa muhula wa tatu mtawalia kuwa ndiye mshindi.




Uchaguzi huo ulikuwa wa aina yake kwani Rais wa sasa Nicolás Maduro, picha na jina lake vilionekana mara tisa (9) kwenye karatasi ya kupigia kura. Kiongozi wa upinzani ambaye ndiye alikuwa mpinzani mkuu wa Maduro, Bi Maria Corina Machando na kuondolewa kwenye papatu za kuwania urais amesema ushindi wa Edmundo González ulikuwa mkubwa akimaanisha kuwa Maduro ameshindwa katika uchaguzi huo.


"Wavenezuela na ulimwengu mzima unajua kilichotokea" mgombea wa upinzani Edmundo González alisema kwenye kauli yake ya kwanza baada ya matokeo kutangazwa. Baraza la taifa la uchaguzi la nchi hiyo ambalo kwa kiasi kikubwa linashutumiwa kuwa na idadi kubwa ya viongozi ambao ni wafuasi kindaki wa rais Nicolás Maduro awali walisema Maduro amepata 51% huku mpinzani wake akipata 44% ingawa baraza hilo halikutoa idadi ya kura kutoka kila kituo na kuahidi kufanya hivyo ndani ya saa chache zijazo.


Kufuatia matokea hayo viongozi mbalimbali wamekuwa na maoni mseto kwani wapo waliopongeza ushindi wa Maduro huku wengine wakitaka uthibitisho wa kupata karatasi zinazonesha idadi halisi ya kura kutoka katika kila kituo ili kupata ujumisho ulio sahihi.


Viongozi wengi waliopongeza ushindi wa Maduro ni wale wenye mfumo wa kijamaa katika nchi zao ambazo zinapinga mfumo wa kibepari (capitalism). Argentina, Bolivia na Cuba ni miongoni mwa nchi zilizopongeza ushindi wa maduro. Marekani, Italia na nchi zote za magharibi zimeonesha shaka juu ya uhalali wa matokeo hayo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page