top of page

URUSI YAJIBU VITISHO VYA TRUMP DHIDI YA NCHI ZA BRICS KUWEKEWA USHURU WA 100%

Na VENANCE JOHN


Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imetoa taarifa kuhusiana na tishio la Rais wa Marekani Donald Trump la kutoza ushuru wa asilimia 100 kwa bidhaa zinazoagizwa Marekani kutoka nchi zinazounda muungano wa BRICS iwapo dola itafutwa katika mabadilishano ya kibiashara ya nchi hizo.


Taarifa ya Urusi imesisitiza kuwa ushirikiano wa nchi wanachama wa BRICS unalenga kuimarisha uwezo wa kijamii, kiuchumi na kibinadamu wa nchi hizo.

Itakumbukwa kuwa Rais Trump alitangaza Januari 30 kwamba Marekani itatoza ushuru wa asilimia 100 kwa bidhaa kutoka nchi za BRICS akisisitiza kuwa Marekani haitaruhusu dola kutelekezwa katika biashara ya kimataifa


Katika kujibu tishio la Trump, Msemaji wa ikulu ya Urusi Kremlin, Dmitry Peskov, ameashiria matamshi ya Rais Vladimir Putin wa Urusi, ambaye awali alisema kuwa hakuna mipango yoyote ya kuunda sarafu ya pamoja katika kundi la BRICS, na kwamba limeazimia kuunda majukwaa mapya ya uwekezaji ambayo yataruhusu uwekezaji wa pamoja katika nchi za ulimwenu wa tatu ( nchi zinazoendelea). Nchi zinazounda BRICS ni Brazil, Urusi, India, China, Afrika Kusini, Iran huku nchi nyingine kama Nigeria zikiwa ziko kwenye mchakato wa kuomba kuwa wanachma wa muungano huo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page