top of page

UWEPO WA TIKTOK MAREKANI WAZIDI KUWA MASHAKANI...

Rais wa Marekani Joe Biden amesaini Muswada unaopendekeza kufungiwa kwa Mtandao wa #TikTok unaomilikiwa na Kampuni ya ByteDance ya China endapo itagoma kuuzwa na kumilikiwa na kampuni za Marekani




Kufuatia hatua hiyo, ByteDance itakuwa na takriban siku 270 kukamilisha mauzo ya TikTok pia inaweza kuongezewa siku 90 na Rais kufikisha Mwaka mmoja tu wa kuepuka kufungiwa nchini Marekani

Hata hivyo, ByteDance imesema itafungua kesi ya kupinga utekelezwaji wa Sheria hiyo huku ikidai utawala wa Biden unataka kuminya uhuru wa Wamarekani zaidi ya Milioni 170 wanaotumia Tik Tok

Kwa mujibu taarifa za Serikali ya Marekani, Tik Tok inadaiwa kuhatarisha Usalama wa Taarifa Binafsi za Watumiaji pamoja na uwezekano wa kuingilia na kuvuruga Masuala ya Kiusalama ikiwemo Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.

Komentarze


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page