Mwanadada Vera Sidika kutoka nchini Kenya amefanya kufuru ya Sherehe kubwa ya
![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_d5cccb86bfa042cabb8ecb542f01ad05~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_d5cccb86bfa042cabb8ecb542f01ad05~mv2.jpg)
kusherehekea kuachana na mumewe msanii Brown Mauzo ambapo ndani ya Sherehe kulikuwa na kila aina ya Starehe ikiwemo kuharibu haribu keki yenye mfano wa harusi.
Vera amesema kufanya Sherehe ya kuachana kwake ni bora kabisa kuliko kwenda kupata tiba kutoka kwa wataalamu wa saikolojia (Therapy).
Brown Mauzo na Vera Sidika wamejaaliwa watoto wawili. Ikumbukwe kuwa ndoa yao ilivunjika mwezi Agosti mwaka jana 2023.
NB: Video ya Sherehe hatujaiweka hapa kwa sababu ya kimaadili.
Comments