top of page

VITENDO VYA UBAGUZI DHIDI YA WAISLAMU KATIKA BARA LA ULAYA VYAKITHIRI - SHIRIKA LA HAKI ZA MSINGI LA ULAYA (FRA)

Na Ester Madeghe,


Watu wa dini ya Kiislamu barani Ulaya wameendelea kuandamwa na vitendo vya chuki na ubaguzi katika mataifa hayo yanayopigia debe au kuweka nguvu kubwa katika uhuru wa kusema na kuabudu.


Ripoti zinaonyesha kuwa, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya bado vinaendelea na moja ya matokeo yake ni kuimarika kwa tabia za kibaguzi na ubaguzi wa rangi dhidi ya jamii ya Kiislamu katika bara hilo.


Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa, nusu ya Waislamu katika mataifa mbalimbali ya Ulaya walitusiwa au kubaguliwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwa uchache.


Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo uliofanywa na Shirika la Haki za Msingi la Ulaya (FRA) kuhusu ubaguzi dhidi ya Waislamu katika Umoja wa Ulaya, Waislamu nchini Ujerumani wamekumbwa na ubaguzi mkubwa zaidi wa rangi kuliko Austria.


Mpaka sasa kumekuwa na ushambuliaji wa misikiti na vituo vya kidini vya Kiislamu, kuwanyanyasa Waislamu wanaovaa mavazi ya Kiislamu, na kukosekana usawa katika upataji ajira na elimu ni mifano hai ya mashinikizo yanayowaandama Waislamu katika nchi za Ulaya.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page