Mbunge wa kuteuliwa Shamsi Vuai Nahodha ameshauri mfumo wa elimu ubadilishwe kutokana na mfumo wa elimu wa Tanzania kutokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na kupunguza umaskini

Ameyasema hayo wakati akichangia mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali wa mwaka 2025/26. Aidha amesema kuwa njia muafaka ya kuongeza tija katika uzalishaji iwe katika sekta ya kilimo au viwanda hivyo elimu bora ipaswe kuwa ya ufundi na ugunduzi
“Ni bahati mbaya elimu yetu haikidhi kiwango bora cha uzalishaji na mara nyingi tunafundisha masomo ya jumla badala ya yanayosisitiza ujuzi, weledi na umahiri, tunatumia wastani wa Sh. bilioni 500 kila mwaka kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu na fedha hizi mchango wake ni mdogo katika kukuza uchumi”.
留言