top of page

WAANDAMANAJI WACHOMA MOTO NYUMBA YA FAMILIA YA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA BANGLADESH

Na VENANCE JOHN


Waandamanaji nchini Bangladesh wameharibu na kuchoma moto nyumba ya zamani ya familia ya waziri mkuu aliyeondolewa madarakani Sheikh Hasina, pamoja na zile za wanachama wengine wa chama chake.


Machafuko hayo yalisababishwa na habari kwamba Hasina angehutubia nchi hiyo kupitia mitandao ya kijamii akiwa nchini India, ambako amekuwa uhamishoni tangu maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi yalipomtoa madarakani mwaka jana.


Hasina mwenye umri wa miaka 77, ambaye aliiongoza Bangladesh kwa miaka 20, alionekana kama mbabe ambaye serikali yake iliwabana wapinzani bila huruma. Jana jioni, Tingatinga (excavator) lilivunja nyumba ya marehemu babake Hasina, Sheikh Mujibur Rahman, ambaye pia ni rais mwanzilishi wa Bangladesh.


Babake Hasina anatazamwa sana kama shujaa wa uhuru, lakini hasira dhidi ya bintiye imeharibu urithi wake kati ya wakosoaji wa Hasina. Kupitia mtandao wa facebook, Sheikh Hazina alilaani tukio hilo akisema; "wanaweza kubomoa jengo, lakini hawawezi kufuta historia."


Hasina, aliyewahi kusifiwa kama kigogo wa demokrasia, ameona sifa yake kuwa mbaya baada ya kuchukua wadhifa huo. Ameshutumiwa kwa kuiba uchaguzi na kuwafunga wakosoaji wake, na utawala wake ulionekana kuwa fisadi. Wakati Hasina alikimbilia India Agosti mwaka jana, hasira bado haijaisha dhidi yake na washirika wenzake wa chama wa Awami League.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page