top of page

WAASI WA M23 WALITEKA JIJI LA GOMA, RAIS RUTO WA KENYA AITISHA KIKAO CHA DHARURA

Na VENANCE JOHN


Waasi wanaoungwa mkono na Rwanda wamesonga mbele katika uwanja wa makabilano mpaka katikati mwa jiji kubwa zaidi mashariki mwa Kongo la Goma siku ya leo Jumatatu. Muungano wa waasi, unaoongozwa na wanamgambo wa kabila la Watutsi wanaoongozwa na M23, umesema umeteka mji mzima wa kando ya ziwa, lakini hilo bado ni ngumu kuthibitishwa kwa uwazi.


Milio ya risasi imesikika karibu na uwanja wa ndege, katikati mwa jiji na mpaka na Rwanda. "Kuna mkanganyiko mjini. Hapa karibu na uwanja wa ndege, tunaona wanajeshi. Bado sijaona M23," mkazi mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters kwa simu, akiomba kutotajwa jina.


Corneille Nangaa, kiongozi wa Muungano wa Mto Kongo unaojumuisha M23, ameliambia shirika la habari la Reuters leo kwamba vikosi vyake vinadhibiti Goma na kwamba wanajeshi wa seikali walikuwa wakisalimu amri kwa kuweka silaha chini.


Hata hivyo, mwenyekiti wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Tryphon Kin-Kiey Mulumba, amesema jeshi la serikali bado linashikilia uwanja wa ndege.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema Rwanda imetuma wanajeshi 3,000 mpaka 4,000 na kutoa nguvu kubwa kwa M23, ikiwa ni pamoja na makombora na wadunguaji kulisaidia kundi hilo. Rais wa Kenya William Ruto, mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo anafanya mkutano wa dharura kwa wakuu wa nchi kuhusu hali hiyo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page