Na VENANCE JOHN
Wabunge watano wa chama cha Democratic nchini Marekani kutoka siku ya jana Alhamisi wamesema walilengwa kwa vitisho vya bomu nyumbani kwao, lakini hakuna vilipuzi vilivyopatikana, kulingana na mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya ndani.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_45c88ec4e51b4e18a6884b7023c20150~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_45c88ec4e51b4e18a6884b7023c20150~mv2.jpeg)
Wawakilishi wa Marekani Jim Himes, Jahana Hayes, John Larson na Joe Courtney, wote kutoka Connecticut, waliripoti vitisho hivyo katika ya jana ambayo ilikuwa siku ya kutoa shukrani.
"Hakuna mahali pa vurugu za kisiasa katika nchi hii, na ninatumai kuwa sote tunaweza kuendelea na msimu wa likizo kwa amani na ustaarabu," alisema Himes.
Naye Hayes alisema, “polisi walimwambia walipokea barua pepe iliyosema kwamba bomu la bomba lilikuwa limewekwa kwenye sanduku la barua nyumbani kwangu, lakini hakuna mabomu au vilipuzi vilivyopatikana na kwamba uchunguzi unaendelea”.
Vyombo vya habari vya eneo la Connecticut viliripoti kwamba Seneta wa Marekani Chris Murphy, kutoa chama cha democrat, pia alikuwa akilengwa. Polisi wa bunge la Marekani hawakujibu mara moja ombi la kutoa ufafanuzi wa jambo hilo walipotafutwa na shirika la habari la Reuters. Wataalamu wa utekelezaji wa sheria wanaona kuwa ni aina ya vitisho au unyanyasaji ambayo inazidi kutumiwa kuwalenga watu mashuhuri.
Comments