Na VENANCE JOHN
Wapalestina 90 wameachiwa huru kutoka jela la Ofer lililoko katika Ukingo wa Magharib. Kuachiwa kwa mateka hao ni sehemu ya kutimiza makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza yaliyofikiwa kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas wiki iliyopita.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_40afac3addce4c98ad2b218fc552d45a~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_40afac3addce4c98ad2b218fc552d45a~mv2.jpeg)
Mabasi mawili yaliyokuwa yamewabeba wafungwa hao yalipokelewa na umati wa watu waliokuwa wamejawa na furaha Gaza. Hamas inasema kwa kila mateka wa Israel aliyeachiliwa huru, wafungwa 30 wa Kipalestina wataachiwa kutoka jela za Israel.
Wengi wa wafungwa walioachiwa huru ni wanawake na inatarajiwa takriban wapalestina 2000 wataachiwa huru katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa makubaliano hayo. Pia zaidi ya malori 630 yaliyobeba bidhaa za misaada, yameruhiswa kuingia Gaza.
Wakati mpango wa kusitisha mapigano ukisherehekewa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonya kwamba kushughulikia mahitaji makubwa ya kiafya ya walioko Gaza itakuwa kazi ngumu itakayokabiliwa na changamoto.
Comments