![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_22f2153edff34e2ca37f1722ace71d64~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_22f2153edff34e2ca37f1722ace71d64~mv2.jpg)
.Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na jeshi la uhamiaji limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 16 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Watuhumiwa hao wamekamatwa eneo la msitu Luganga Wilayani Mufindi wakiwa wametelekezwa kwenye shamba la mahindi baada ya kushushwa kwenye gari aina ya Land cruiser V8 yenye namba usajili T 803 CVW ambalo awali ilisomeka namba za usajili STL 3999
Akithibitisha kutokea kwa tukio Hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACAP Allan Bukumbi amesema tukio Hilo lilitokea mnamo tarehe 6.4.2024 Wilayani Mufindi na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa Sheria na taratibu za nchi.
Comentários