top of page

WAKATALIWA KUSAJILI VYAMA 10 VYA SIASA VYOTE VIKIWA NA NENO GEN-Z

Na VENANCE JOHN


Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini Kenya imetuplia mbali majina 10 ya vyama vya siasa vilivyohitaji kutumia neno Gen-Z katika majina yao, akidai kuwa vyama hivyo vimekosa ujumuishi. Mwombaji aliyetambulika kwa jina la Simon Maina Mwangi alifikiria kusajili vyama vya siasa 10 vinavyohusiana na Gen - Z. Majina pendekezwa yalikuwa kama ifuatavyo.




Gen-Z Movement, Gen-Z National Movement, Gen Z Alliance Movement, Gen-Z Democratic Movement, Gen-Z People's Alliance, Gen Z United Movement, Gen-Z People's Movement, Gen-Z Political Party, Gen Z Democratic Party na Gen-Z Alliance Party.


Katika taarifa yake, Msajili wa vyama vya siasa nchini humo Ann Nderitu akifanya rejea ya sheria, amesema kwamba maombi hayo yamevunja Katiba ya Kenya kwani kwa mujibu wa Ibara ya 91 (1) (a) (e) maombi hayo hayawezi kuidhinishwa.


Ibara ya 91(1) (a) inasema kuwa chama cha siasa kinapaswa kuwa na taswira ya kitaifa na sio kundi fulani la watu walio eneo fulani. Huku Ibara ndogo (e) inataka chama chochote cha siasa kuheshimu na kuruhusu watu wote kushiriki kwenye mchakato ikijumuisha walio wachache na hata makundi maalum.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page