Na VENANCE JOHN
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa ana mipango ya kuandaa kituo cha kushikilia wakimbizi katika gereza la kijeshi la Guantanamo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_c9ea52d0a7ab47e0adf89aad79b2c8d3~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_c9ea52d0a7ab47e0adf89aad79b2c8d3~mv2.jpeg)
Trump amesema kituo hicho kitakuwa kwa ajili wakimbizi wapatao karibu 30,000. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Trump kudhibiti uhamiaji haramu. Kituo hicho, ambacho ni tofauti na gereza lenye ulinzi mkali, kimetumika hapo awali kuhifadhi wakimbizi, wakiwemo raia kutoa Haiti na Cuba waliokamatwa baharini.
Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, amesema mipango ya Trump ni ukatili, akidai kuwa wakimbizi hao watawekwa karibu na vituo vilivyotumika kwa mateso na vifungo vinavyokiuka sheria.
Comentarios