top of page

WAKITAKA KUSEMA TUMEZIONEA TIMU DHAIFU MSIMUUNAKUTA TIMU YAO TUMEIKANDA GOLI 7

Wakati Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 ikitamatika leo Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga SC Simon Patrick amefunguka haya kupitia ukurasa wake wa Instagram


"Mambo 5 ya kufungia msimu yanayotufurahisha wananchi;



1. Wakitaka kusema tumezionea timu dhaifu msimu huu unakuta timu yao tumeikanda goli 7 na kukusanya point 6.

2. Wakitaka kumlinganisha Aziz Ki na mchezaji waliotaka

awe mfungaji bora, unakuta Aziz Ki ndiye kinara wa magoli na kawakanda mechi zote.

3. Wakitaka kujiita wajuaji wa mechi za kimataifa unakuta timu yao haitashiriki klabu bingwa msimu ujao.

4. Wakitaka kusema mafanikio yao msimu huu unakuta wana WhatsApp channel na kibegi kama mafanikio.

5. Wakitaka kusema Mzee awaachie timu yao wanakuta timu ishanunuliwa kitambo kwa mujibu wa taarifa ya mnunuzi.

Kwa ufupi timu yao imefeli vita zote msimu huu, vita ya ubingwa, vita ya nafasi ya pili na vita ya mchezaji wampendao kutwaa kiatu cha ufungaji bora.

NB: Muda wa kutumia ile 20B umefika sasa Manzoki aje kuokoa jahazi laa sivo mtaendela kuteka wachezaji Airport".

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page