top of page

WAMEFUZU WATU WASHAMBA SEMBUSE SISI-

WAMEFUZU WATU WASHAMBA SEMBUSE SISI- AHMED ALLY

Kutoka kwa Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amesema

"Jumamosi tunakwenda kuingia robo fainali kwa mara ya tano mfululizo, kwetu sisi kuingia robo ni jambo la kawaida. Tumezoea kucheza robo na hatujawahi kuishia makundi tangu tumeanza kampeni yetu ya kimataifa."

"Tulimuua AS Vita wa moto, tulimuua USGN, tulimuua Horoya hatuwezi kushindwa kwa Jwaneng Galaxy. Simba anapoitaka robo fainali hakuna wa kutuzuia hata timu zingine zote duniani zitengeneze timu moja. Jwaneng amekuja wakati mbaya, muda ambao tunataka kulipiza kisasi."

"Lilitukaa rohoni lakini muda wa kumtemea nyongo Jwaneng Galaxy, tulikaa na maumivu kwa miaka mitatu na la pili tunataka kuingia robo fainali. Hatuwezi kufungwa na timu inayoburuza mkia katika kundi letu."

"Tutafanya kila kinachowezekana ilimradi Simba ipate ushindi siku hiyo na hakuna kinachoshindikana. Iwe ardhini, angani au chini ya bahari."

"Tunawaahidi na kuwahakikishia Wanasimba kama kuna kitu kinahitajika hata kiwe kinapatikana chini ya bahari tutakifanya ili Simba iende robo fainali. Jumamosi ni kwenda kumalizia kazi."

"Robo fainali wamefuzu watu washambawashamba sembuse sisi. Hatuwezi kushindwa kwenda robo fainali, yani waporipori wamefuzu alafu sisi wenye mashindano tushindwe? Jumamosi saa 1 usiku tunakutana kumaliza kazi."- Ahmed Ally.

Comentários


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page