Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Msigwa ametoa Ufafanuzi wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusilukia juu ya watumishi wa Umma mkoa wa Dar es Salaam kufanyia kazi nyumbani kuanzia Januar 27 hadi 28 kupisha mkutano wa Nishati wakuu wa Nchi wa Bara la Afrika. Msigwa kupitia mtandao wake wa "X" zamani Twitter ameandika
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_29df72df91bc4fbdbbb218b63207bb7f~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_29df72df91bc4fbdbbb218b63207bb7f~mv2.jpeg)
"Kufuatia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi kuwa tarehe 27 na 28 Januari, 2025 Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Dar es Salaam wafanyie kazi nyumbani kutokana na barabara nyingi kufungwa ili kupisha Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Barani Afrika, mnajulishwa kuwa Wanafunzi wa shule na vyuo pia mnapaswa kusomea nyumbani kwa siku hizo mbili. Taasisi za sekta binafsi mnashauriwa kufanya vivyo hivyo ili kuepusha usumbufu ambao wafanyakazi na wanafunzi wanaweza kuupata."
Comments