Na VENANCE JOHN
Mahakama yakijeshi Nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC imefunguwa kesi mjini Bukavu dhidi ya askari 84 wa jeshi la nchi hiyo wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya watu wasiopungua 9 wilayani Kabare na kuporaji mali za raia.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_857f444040d1487184edb7d75b725f87~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_857f444040d1487184edb7d75b725f87~mv2.jpeg)
Baadhi ya askari hao ni wa kikosi kinachoitwa Duma au Guépard, wakituhumiwa kwa mauaji, wizi, uporaji, uasi, kumtoroka adui, ubakaji na kadhalika. “Mimi nigependa kutendwa haki, watu hao wafungwa kwa sababu hawakuchagua mtoto wala mtu mzima.” Anasema Mugoli Alice Civarara ambaye ni mkazi wa Cirato katika kijiji cha Kavumu.
Jumamosi, askari wenye silaha walipora maduka na masoko madogo madogo pia mjini Bukavu na kufyatua risasi hewani. Hali hii pia ilishuhudiwa katika kijiji cha Nyangezi Jumapili jioni, wakazi wengi wa vijiji tangu Katana hadi Mumosho wakitoa malalamiko.
Jeshi la Congo DR linasema linasikitishwa na hali hii, na linathibitisha kukamatwa kwa askari hao waliotoka vitani na waliofanya maovu hayo dhidi ya raia. Meja Nestor Mavudisa ni msemaji wa eneo la tatu la ulinzi nchini Kongo, anasisitiza kuwa jeshi la Kongo halitawavumilia askari wasio na nidhamu ambao wanachafua sura ya jeshi hilo.
Comments