Na VENANCE JOHN
Ufaransa na Senegal zinaweka masharti ya kuwaondoa wanajeshi wote wa Ufaransa walioko katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2025.
Nchi hizo mbili zimesema katika taarifa yake kwamba zinaunda tume ya pamoja ambayo itasimamia kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa kutoka nchi hiyo na kurejesha vituo vya kijeshi ifikapo mwisho wa mwaka. Wizara za mambo ya nje za nchi zote mbili zimesema zinakusudia kufanyia kazi ushirikiano mpya wa ulinzi na usalama ambao utazingatia "ipaumbele vya kimkakati vya pande zote.
Mwezi Novemba, Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye alitangaza kwamba kambi za jeshi la Ufaransa haziendani na uhuru wa nchi na wanajeshi wake 350 wanapaswa kuondoka. Hatua hiyo imekuja muda mfupi kabla ya Senegal kuadhimisha miaka 80 ya mauaji ya halaiki ya wanajeshi wa Afrika Magharibi yaliyofanywa na wakoloni mwaka 1944.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekiri katika barua kwa Faye mwaka jana kwamba Ufaransa ilifanya mauaji. Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa Januari, Ufaransa ilikamilisha kuondoa wanajeshi wake kutoka nchi ya Chad wakati Ivory Coast ilitangaza mapema kuondoa vikosi vya Ufaransa.
Comments