top of page

WANASAYANSI WAGUNDUA HIFADHI YA MAJI KATIKA MIAMBA YA SAYARI YA NNE (4)

Na VENANCE JOHN


Wanasayansi wa anga za juu wa Marekani wamegundua hifadhi ya maji katika miamba ya Martian iliyopo ndani ya sayari ya nne (4) ya mirihi (Mars).


Ugunduzi huo unakuja baada ya uchambuzi wa data kutoka shirika la anga za juu la Marekani NASA ambalo lilipeleka kifaa cha Seismomita (seismometer) kufanya uchunguzi wa mtetemeko wa miamba ya sayari hiyo.


Wanasayansi hao wamegundua hifadhi hiyo ya maji inapatikana kina kirefu ndani ya kokwa la juu (crust) la mwamba unaopatika kwenye sayari hiyo. Kokwa la juu ni ukanda wa juu kabisa ambao kama ingekuwa kwenye sayari ya dunia ni sawa na ardhi ya juu. Hii ni mara ya kwanza kugundulika kwa maji kwenye sayari hiyo nyekundu, na kuleta ushahidi kwamba miamba ya Martian inayopatikana kwenye sayari ina hifadhi ya maji.


"Hizi ndizo njia sawa tunazotumia kuchunguza maji ya aridhini, gesi na mafuta katika sayari ya dunia", ameelezea Profesa kutoka chuo kikuu cha California, Prof. Michael Manga ambaye alikuwa sehemu ya utafiti huo. Uchambuzi wa data umegundua kuwa, hifadhi ya maji iko umbali wa kina cha karibu maili 12 (kilomita 10-20) kutoka juu ya uso wa mwamba.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page