Kutoka kwenye ukurasa wa Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amefunguka haya baada ya Klabu yake kuachana na kocha wao Benchikha
"Moja kati ya Kocha bora kuwahi kuwa nao Simba Sports

Haikua rahisi kumpata Mwalimu wa kaliba yake na hakuna aliyeamini kama tungemudu kuwa na kocha wa aina hiyo
Kumpata Mwalimu huyu ni ishara kuwa viongozi wetu walionesha dhamira ya dhati ya kuipeleka Simba kwenye kilele cha mafaniko makubwa zaidi
Ukubwa wa Mwalimu Benchikha na gharama za kuwa na Mwalimu wa aina yake ni dhahiri kuwa viongozi wetu wakiongozwa na @moodewji walijitoa mhanga kwa maslahi ya kuiboresha Simba yetu Juhudi ya kwanza ilikua ni kumleta Kocha jambo ambalo limefanyika kwa asilimia mia juhudi ya pili ilikua ni kubaki nae Kocha kubaki kazini au Muajiriwa yeyote kubaki kazini hutegemea pia na matakwa ya muajiriwa binafsi Wana Simba tutulie tuwape muda viongozi wetu watafute Kocha mwingine mzuri kwa maslahi ya timu, Kama waliweza kumleta Benchikha basi wanaweza kuleta yeyote mzuri kwa maslahi ya Simba yetu
Maisha yanaendelea!!". Ahmed Ally.
Comments