Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Mb.) amewataka wanawake wote nchini kushikama katika kuilea jamii ya watanzania ili kujenga jamii iliyo staarabika katika nyanja zote za maendeleo endelevu ya Taifa.
Mhe. Pinda amesema hayo tarehe 21 Desemba 2024 katika alipokuwa mgeni rasmi hafla ya uzinduzi wa kitabu cha NGUVU YA MALENGO iliyofanyika katika ukumbi wa Cavillan Social Hall Jijini Dodoma.

"Wamama mimi niendelee kuwapongeza msirudi nyuma mnatulisha familia zetu zinaishi kwa migongo yenu nyingi sana" amesema Naibu Waziri Mhe.Pinda "Kwa hiyo ni wapongezee wamama, wamama kaza kamba tusaidieni tuleeni" ameongeza Mhe. Pinda
Aidha mhe. Pinda amewataka watanzania kote nchini kuunga jitihada za maendeleo za Serikali ya awamu ya sita iliyoko chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan. "Mama Samia ni nguvu ya malengo ya nchi yetu kwa sababu alichokilenga anataka kifike na aone matokea yake" amesema Naibu Waziri mhe. Pinda
Ameongeza kuwa dhamira ya dhati ya Rais Samia ya kuwaletea wananchi Maendeleo imeleta mabadiliko makubwa ndani na nje ya nchi kwa kuendeleza miradi ya kimkakati ya watangulizi wake katika awamu zilizopita.
Comments