top of page
Radio on air

WAPALESTINA MILIONI 2.5 HATARINI GAZA

Na mwandishi wetu Venance John

Umoja wa mataifa umesema wapalestina milioni 2.5 Kusini mwa Gaza wameathiriwa  na



tangazo lililotolewa na jeshi la Israeli likiwataka kuhama eneo hilo.

Watu wengi wamekuwa wakiingia eneo la Khan Younis  kwa mguu na kwa magari wakitoka maeneo mbalimbali kukimbia mapigano kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wanamgambo wa Hamas

Wagonjwa na wafanyakazi wa wameanza pia kuikimbia hospitali kubwa katika eneo hilo ingawa jeshi la Israel limesema hawakuwa welengwa wa amri ya kuhama

Maafisa wa afya wa Gaza wanasema Wapalestina nane wameuawa na dozeni ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya usiku wa kuamkia siku ya jumanne

Louise Wateridge afisa wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi wa Wapalestina UNRWA amewaomba watu waondoke kwa kuwa wamelazimika kuyaacha tena makazi yao.


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page