![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_b57915e74a084fa68b9dd83f4c3f79b2~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_b57915e74a084fa68b9dd83f4c3f79b2~mv2.jpg)
Mijengo ya Diddy huko Miami na Los Angeles ilivamiwa na maafisa Usalama mnamo Machi, huku watoto wake wakifungwa pingu wakati wa uvamizi huo. Uvamizi huo mkubwa ulitokea huku ukionekana moja kwa moja kwenye TV na iliripotiwa kuhusishwa na uchunguzi wa ulanguzi wa ngono(sex trafficking). Diddy hakuwa kwenye majengo wakati huo, na inadaiwa alikodi ndege kwenda Bahamas kwa likizo ya familia pamoja na binti zake. Diddy alionekana akizungumza na wachunguzi huko Florida, lakini hakukamatwa.
Wakati wa uvamizi huo, mamlaka ya zilishikilia vifaa vyake vyote vya kielektroniki na silaha mbalimbali alizokuwa nazo. Polisi pia walimkamata Brendan Paul, ambaye alishutumiwa kuwa mshirika wa muda mrefu wa Diddy kwenye ulanguzi wa dawa za kulevya.
J. Cole
J. Cole sio rapa wa kwanza unayeweza kumfikiria linapokuja suala la kuvamiwa na polisi lakini lilimtokea Machi 18, 2016. Wakati MC na crew yake ya Dreamville Records walikuwa chini mjini Austin, Texas kwa ajili ya Tamasha la Kila mwaka la SXSW, studio yake ya North Carolina iliweA inavamiwa na kikosi cha SWAT waliokuwa na silaha.
Uvamizi huo ambao ulinaswa na kamera, unaonyesha maafisa 12 wa kikosi cha SWAT wakikaribia nyumba hiyo na kuvunja mlango, huku mmoja wa maafisa akiondoa kamera iliyokuwa ikirekodi fiasco. Wakichukua ushauri usio na ushahidi kutoka kwa jirani ambaye aliamini kwamba Cole na marafiki zake walikuwa wakijihusisha na biashara ya madaw ya kulevya aina ya marijuana bangi na wakitumia nyumba hiyo kama sehemu ya kuhifadhia.
Polo G
Polo G nyumba yake ilivamiwa na polisi mnamo Agosti 2023. Video ya uvamizi huo iliyonaswa na TMZ ilionyesha kundi la polisi wakiwa wamevalia mavazi la kujilinda mbele ya nyumba ya rapper huyo wa Chicago, iliyoko Los Angeles. Watu wengi walionekana wakitoka nje ya nyumba hiyo, akiwemo Polo G, ambaye alitoka akiwa pingu mkononi. Polisi walikuwa wameripotiwa kutekeleza agizo la upekuzi kwenye nyumba hiyo inayohusiana na wizi. Watu wanne waliwekwa kizuizini. Haijabainika iwapo kuna yeyote alikamatwa kufuatia upekuzi katika nyumba hiyo.
"Inajulikana sana kwamba polo si mhalifu aliyehukumiwa na hakuwahi kuwa mhalifu," wakili wa polo Bradford Cohen alisema kwenye taarifa. "Mimi binafsi nilipata mashtaka yake yote huko Miami7 yakitupiliwa mbali wakati kwa maoni yetu tukisisitiza alikamatwa kimakosa na kushtakiwa."
Young Thug
Kabla ya kesi ya YSL RICO kusitishwa, Young Thug alikamatwa nyumbani kwake kwa kibali ambacho hakijalipwa mnamo Julai 15, 2015. Wakati wa kukamatwa kwake, nyumba yake pia ilivamiwa, huku maafisa wakikuta dawa za kulevya na bunduki kwenye majengo. Alishtakiwa siku iliyofuata kwa mashtaka mbalimbali ya uhalifu, madawa ya kulevya na silaha, lakini Thugger angeachiliwa kwa dhamana ya $ 10,000. Hatimaye, mashtaka yote dhidi yake yalitupiliwa mbali baada ya uvamizi wa awali wa nyumba yake kuonekana kuwa kinyume cha sheria.
Lil Wayne
Mnamo Novemba 3, 2015, polisi walivamia jumba la kifahari la Lil Wayne lililoko Miami Beach wakiwa na hati ya ushuru, ambayo hutumiwa kushikiliq mali, kutokana na madeni ambayo hayajalipwa kuhusiana na uamuzi wa jaji kwamba rapper huyo aagizwe kulipa dola milioni 2 kwa kampuni ya Ndege ya Leasing Signature Group.
6ix9ine
6ix9ine ambaye alikuwa na mjengo wake Brooklyn ilivamiwa mwaka wa 2018. Haikuwa wazi ni nini kilisababisha msako huo, lakini polisi walihisi kuwa kuna silaha inamilikiwa isivyo halali na rapa huyo. Polisi hawakuwa na uhakika kama bunduki hiyo ilikuwa ya 6ixe9ine kwani rapper huyo alikuwa hajarejea nyumbani kwake kwa muda kidogo. Zaidi ya hayo, chanzo karibu na 6ix9ine kiliiarifu TMZ kuwa anaripotiwa kuwa katika harakati za kuhama nyumba hiyo.
Bobby Shmurda
Uvamizi mwingine kuwahi kutokea katika kwa wanamuziki wa hip-hop ulitokea tarehe 18 Desemba 2014, kwa mwanamuziki na rapa kutoka Brooklyn Bobby Shmurda na memba wa kundi lake la GS9 walipokamatwa studioni Quad Studios huko Manhattan, N.Y. kutokana na uchunguzi wa muda mrefu. Uvamizi huo ambao ulipata umaarufu sana ukimuhusisha Bobby Shmurda, umiliki w bunduki 21, ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya cocaine na bangi. Bobby Shmurda alihukumiwa kutokana na kupatikana na hatia huku akiachiwa huru mnamo Februari 2021.
Gucci Mane
Mjengo wa raapa kutoka Atlanta, Georgia "Waka Flocka Flame" huko Georgia ilivamiwa mnamo Desemba 2010. Uvamizi huo ulihusiana na uchunguzi wa uwezekano wa uwepo wa biashara ya ngono na ushahidi wa bunduki na dawa za kulevya katika eneo hilo. Na ingawa Waka Flocka hakuwa nyumbani wakati wa uvamizi huo, rapper Gucci Mane alikuwa, kwani aliishi na Waka na mama yake kwa muda.
Gucci alifungwa pingu baada ya polisi kupata silaha na kiasi kidogo cha bangi kwenye eneo la tukio, lakini angeachiliwa baadaye. Mamake Waka Flocka pia angedai kuwa polisi walikuwa wakitafuta ushahidi wa mwanawe kuwa na uhusiano na magenge yoyote ya kihalifu.
Nipsey Hussle
Nipsey Hussle alitarajiwa kupiga kuingia kuingia kwenye stage katika show yake ya "Made in America la 2014, lakini msako wa polisi uliotokea saa chache kabla ya onyesho lake lililoratibiwa kukatiza mipango hiyo. Mnamo Agosti 29, 2014, LAPD ilifika katika eneo la Slauson Avenue Clothing katika sehemu ya Hyde Park ya L.A. ili kujibu upekuzi wa malalamiko ya muda wa majaribio, na kumkamata mtuhumiwa waliyekuwa wanamtaka pamoja na Nipsey Hussle. Rapa huyo alikosa onyesho lake lililopangwa siku hiyo, lakini aliweka dhamana ya $ 13,000 ili kuhakikisha kuwa anaweza kupafomu tamasha hilo la Made in America.
Sean Kingston
Jumba la kifahari la Sean Kingston la Southwest Ranches huko Dania Beach, Fla. lilivamiwa na timu ya SWAT inayotoa hati za kukamatwa na kupekuliwa mnamo Mei 23, 2024. Wakati wa uvamizi huo, mamake Janice Turner aliwekwa chini ya ulinzi kwa mashtaka mengi ya ulaghai na wizi. Kingston alikamatwa saa chache baadaye huko California kwa makosa ya ulaghai na wizi pia.
Kukamatwa kwa watu hao kuliripotiwa kuhusiana na Kingston kushindwa kulipia mfumo wa sauti wa televisheni wa $150,000 aliouzwa kutoka Ver Vert Entertainment.
Wengine ni Soulja Boy, Dj Drama, Afroman, Chief Keef, Belly, Suge Knight, Stormzy, T.I, Paul Wall, Turk, Juelz Santana, MoneyBagg Yo, Feature, Gallery, Galleries, Irv Gotti, Trick Daddy na Maxo Kream.
Комментарии