Na VENANCE JOHN
Jiji kubwa la Mya limegunduliwa baada ya karne nyingi za kutoweka katika misitu huko Mexico. Watalaamu wa shughuli za kibidamu na utafiti wa mali kale, (Archaeologists) walipata majengo ya piramidi, uwanja wa michezo, njia kuu zinazounganisha wilaya na ukumbi wa michezo katika jimbo la kusini mashariki la Campeche nchini humo. Timu hiyo ya watafiti iligundua maeneo matatu kwa jumla, ambayo yana ukubwa sawa na mji mkuu wa Scotland, Edinburgh.

"Nilikuwa kwenye kitu kama ukurasa wa 16 wa utafutaji wa Google na nikapata uchunguzi wa uliofanywa na shirika la Mexico kwa ajili ya ufuatiliaji wa mazingira," anaelezea Luke Auld-Thomas, mwanafunzi wa PhD katika chuo kikuu cha Tulane nchini Marekani.
Lakini Bw. Auld-Thomas alipochakata data kwa mbinu zilizotumiwa na wanaakiolojia (Archaeologists), aliona kile ambacho wengine walikuwa wamekosa, ambacho ni jiji kubwa la kale ambalo huenda lilikuwa na watu elfu 30 mpaka 50 katika kilele chake kutoka mwaka 750 mpaka mwaka 850 baada ya Yesu (AD).
Bw Auld-Thomas watafiti wenzake waliamua kuliita jiji hilo Valeriana kana jina la rasi iliyo karibu na eneo hilo. Profesa Marcello Canuto, mwandishi mwenza katika utafiti huo anasema ugunduzi kama huo husaidia kubadilisha wazo katika fikira za Magharibi kwamba nchi za Tropiki ndipo ustaarabu ulipofia na badala yake, kuonesha kuwa sehemu hii ya dunia ilikuwa na tamaduni tajiri na tata.
Wanaakiolojia wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yalikuwa sababu kuu ya kupotea kwa jiji la Maya na sababu nyinginezo kama vita na kutekwa kwa eneo hilo na wavamizi wa Hispania katika karne ya 16 pia kulichangia kutokomea majimbo ya jiji la Maya.
Jiji hilo ambalo limepewa jina la Valeriana na watafiti ho, lina alama za mji mkuu na lilikuwa la pili kwa msongamano wa majengo hadi kuwa eneo la kuvutia. Watafiti hao wanasema, kutoka eneo la jiji hilo lililotoweka ni mwendo wa dakika 15 tu kufika kwenye barabara kuu karibu na Xpujil ambako watu wengi wa Maya wanaishi kwa sasa.
Valeriana ina majengo mawili ya plaza zenye piramidi za hekalu, ambapo watu wa Maya walikuwa wanaabudu, na pia kuna hazina zilizofichwa kama vinyago vya jade. Ushahidi wa magofu hayo ulipatikana na ndege ikitumia rada kuchora ramani chini ya msitu huo.
Comentários