Na Ester Madeghe,
Mamlaka ya Taifa ya Kudhibiti Ukame nchini Kenya (NDMA) imesema kuwa takribani watoto 479,498 wenye umri wa miaka mitano katika maeneo 23 ya ukame nchini humo wanakabiliwa na utapiamlo na wanahitaji matibabu.

Ingawa kesi za utapiamlo zimeendelea kuwa juu, lakini idadi hiyo inaonesha kupungua kutoka 760,488 mwezi Julai. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwezi Septemba ya NDMA iliyotolewa Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, akinamama wajawazito na wanaonyonyesha 110,169 wana utapiamlo na wanahitaji huduma ya haraka ya afya. Kesi za utapiamlo zinatokana na matukio mabaya ya hali ya hewa, kipato cha chini na hduma duni za afya. NDMA pia imebainisha kuwa Wakenya milioni 1 bado wanahitaji misaada ya kibinadamu, idadi ambayo haijabadilika tangu mwezi Julai.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, watoto wapatao milioni 10.8 na karibu wanawake milioni 1 wajawazito na wanaonyonyesha wamekumbwa na utapiamlo na wanahitaji matibabu ya haraka katika Pembe ya Afrika.
Comments