Na VENANCE JOHN
Mlipuko uliotokea katika kiwanda cha kutengeneza risasi na vilipuzi kaskazini-magharibi mwa Uturuki umesababisha vifo vya watu 12 na wengine wanne kujeruhiwa.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_c6a579bf9ab84a43a81b01015fc5bf60~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_c6a579bf9ab84a43a81b01015fc5bf60~mv2.jpeg)
Gavana wa jiji la Balikesir, Ismail Ustaoglu, amesema mlipuko huo umetokea saa 2:25 asubuhi kwa saa za huko katika sehemu ya uzalishaji wa vibonge. Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya amesema sababu bado haijabainika, lakini mamlaka imefutilia mbali kama inaweza kuwa ni hujuma.
Video kutoka eneo la tukio zilionyesha moto ukilipuka kutoka kiwandani, na kuharibu sehemu ya jengo, ikifuatiwa na moshi mweusi. Mlipuko huo umesababisha mitetemeko katika kitongoji chote cha Köteyli.
Wafanyakazi wengi wa zimamoto wametumwa kukabiliana na moto huo na vitengo vya afya na usalama vimetumwa katika eneo hilo. Waziri wa Sheria Yilmaz Tunc amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu kitu kilichosababisha mlipuko huo.
Comments