top of page
Radio on air

WATU 121 WAFARIKI KATIKA TUKIO LA KIDINI INDIA....

Na mwandishi wetu Venance John.

Watu 121 wakiwemo wanawake na watoto wamekufa baada ya kutokea mkanyagano katika



kusanyiko la kidini.

Tukio hilo limetokea katika jimbo la Uttar Pradesh, Kaskazini mwa India ambapo taarifa zinaeleza kuwa wengi wa waliofariki ni wanawake.

Tukio hilio limetokea katika wilaya ya Hathras karibu kilomita 200 kusini mashariki mwa mji mkuu wa India, New Delhi

Mamlaka zimesema kulikuwa na kusanyiko kubwa kwenye eneo la wazi lililoitishwa na kiongozi wa kidini kwa ajili ya tamasha la waumini wa dini ya Hindu wakimkumbuka Mungu wao wa Shiva.

Taifa la India limekuwa likishuhudia matukio mengine kama haya kwenye mikusanyiko ya kidini:

Mojawapo ya ni lile la Januari 2005 ambapo waumini 265 wa madhehebu ya Hindu walikufa na wengine wengi walijeruhiwa katika mkanyagano kwenye hekalu la Mandhardevi katika jimbo la Maharashtra. Mkasa huo ulisababishwa na mterezo kwenye njia ya kuingilia hekaluni,

Tukio jingine ni lile la mwezi Agost mwaka 2008ambapo katika hekalu la Naina Devi jimboni Himachal Pradesh watu 145 wa dini ya Hindu walikufa.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page